Wanafunzi wa kike waliotekwa na kundi la kigaidi la Boko Haram katika eneo la Dapchi nchini Nigeria wamerejeshwa.
Wakaazi wa Dapchi wameiambia BBC kuwa wasichana wengi kati ya 110 waliotekwa na kundi hilo wamerejeshwa na gari la kijeshi la magaidi hao mapema leo asubuhi.
Taarifa rasmi za chanzo cha kurejeshwa kwao hazijafafanuliwa, lakini imeezwa kuwa kuna uwezekano wasichana watano kati yao walipoteza maisha.
Mzazi aliyejitambulisha kwa jina la Kundil Bukar, amesema wanajeshi wanaoaminika kuwa ni wa kundi la Boko Haram walikuja na gari katika mji huo na kuwashusha kwa haraka wasichana hao.
Wasichana hao waliotekwa mwezi mmoja uliopita wanadaiwa kuwa katika hali ya uchovu na waliodhoofika.
Afisa mmoja wa Jeshi la Nigeria anayefanya kazi kwenye kituo kimojawapo cha ukaguzi ameliambia shirika la habari la Reuters kuwa “Boko Haram wamewarudisha wasichana.”