Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Simba (C.E.O), Barbara Gonzalez Septemba 5, 2020 alitangazwa na Bodi ya Wakurugenzi kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Senzo Mazingiza Mbatta ambaye kwa sasa anafanya kazi ndani ya Klabu ya Young Afrucans akiwa kama mshauri mkuu kuelekea kwenye mabadiliko ya klabu hiyo.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa klabu ya Simba SC Simba, Mohamed Dewji, alisema: “Hatujakurupuka kufanya maamuzi wala sio maamuzi yangu, ni ya kikao kwani tulikaa na kuamua kumpitisha Barbara, anakuwa CEO wa kwanza mwanamke. Ni mchapakazi na anaipenda Simba, hivyo tunaamini kila kitu kitakwenda sawa.”

Mwanasiasa wa upinzani aliyepewa sumu apata fahamu
Mbeya City yaweka rekodi Dar es salaam