Uongozi wa klabu ya Young Africans mapema hii leo Agosti 28 ulimtangaza kocha mpya atakaekinoa kikosi chao kuelekea msimu mpya wa ligi kuu ya Soka Tanzania Bara ambao utaanza rasmi Septemba 06.

Uongozi wa Young Africans umemtangaza kocha huyo kupitia kwa Mjumbe wa Kamati ya Usajili ambaye pia ni Mkurugenzi Uwekezaji wa Kampuni ya GSM inayoidhamini klabu hiyo Injinia Hersi Said.

Injinia Said amemtangaza kocha Zlatko Krmpotic raia wa Serbia ambaye ana uzoefu na soka la Bara la Afrika, huku akipita kwenye klabu yenye mafanikio katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati TP Mazembe ya DR Congo.

Kocha Zlatko alizaliwa Agosti 07 mwaka 1958 katika mji wa Belgrade, uliopo nchini Serbia, ila kwa zamani ulikua kwenye nchi maarufu ya Yugoslavia.

Kocha huyu amewahi kucheza soka akianza na kikosi cha vijana cha klabu ya Red Star Belgradeni ya nchini kwao Serbia zamani Yugoslavia kabla ya kupandishwa kwenye kikosi cha klabu hiyo cha wakubwa mwaka 1977. Alicheza nafasi ya beki wa kati.

Kocha Zlatko alicheza kwenye kikosi cha wakubwa cha Red Star Belgradeni kuanzia mwaka 1977 hadi mwaka 1986 sawa na misimu minane.

Akiwa na klabu hiyo kama mchezaji alicheza michezo zaidi ya 200 kwenye michuano ya ndani na nje ya Serbia zamani Yugoslavia.

Baadae alihamia nchini Uturuki na akatumia misimu miwili na Gençlerbirliği (1986-1988), na baadae alirudi nyumbani kwao Serbia na kuitumikia klabu ya AIK Bačka Topola, na kisha alistaafu soka rasmi.

KWA UPANDE WA TIMU YA TAIFA.

Kocha Zlatko aliitumikia timu ya taifa ya Yugoslavia kwenye Fainali za Kombe la Dunia la FIFA mwaka 1982, na kuwa sehemu ya kikosi kilichoiwezesha nchi hiyo kumaliza nafasi ya pili, kwenye Kundi la 5.

Kabla ya hapo Kocha Zlatko alikiongoza kikosi cha vijana chini ya umri wa miaka 21 cha Yugoslavia kutwaa taji la Barani Ulaya *UEFA* mwaka 1978.

KAZI YA UKOCHA.

Kocha Zlatko amefanya kazi katika vilabu kadhaa kwenye nchi 12 tofauti duniani.

Nchi hizo ni Serbia akiwa na klabu za AIK Bačka Topola, OFK Beograd, na Obilić. Sweden (Degerfors IF) , Macedonia (Sloga Jugomagnat), Uturuki (Ankaragücü ), Ugiriki (Paniliakos), Kupro (Nea Salamis), Kazakhstan (Kairat), Kuwait (Kazma), DR Kongo (Don Bosco) na TP Mazembe kama kocha msaidizi, Zambia (ZESCO United), Botswana (Jwaneng Galaxy), na Kusini Afrika (Royal Eagles).

Pia kocha Zlatko amewahi kuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 19 Serbia na Montenegro mwaka (2005), na baadae alikabidhiwa kikosi cha vijana chini ya umri wa miaka 19 cha Serbia kuanzia mwaka 2007-2008.

MAISHA BINAFSI

Mbali na kuwa mzaliwa na raia wa Serbia, kocha Zlatko pia nia raia wa Croatia.

MAFANIKIO

Akiwa na klabu ya Red Star Belgrade kama mchezaji, Zlatko alifanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi ya Yugoslavia *Yugoslav First League* mara tatu na hiyo ilikuwa msimu wa 1979–80, 1980–81 na 1983–84.

Akatwaa ubingwa wa Yugoslav Cup kwama mchezaji mara mbili msimu wa 1981–82 na 1984–85.

MAFANIKIO YAKE KIMATAIFA

Alikuwa sehemu ya kikosi cha Yugoslavia chini ya umri wa miaka 21, kilichotwaa ubingwa wa UEFA mwaka 1978

Msimu wa 2016-2017 alitangazwa kuwa kocha mkuu wa Ligi ya DR Congo.

Msimu wa 2017-2018 alitangazwa kuwa kocha mkuu wa Ligi ya Zambia (Zambian Superleague)

Msimu wa 2018-2019 alitangazwa kuwa kocha mkuu wa Ligi ya Botswana.

Shirikisho la soka Afrika CAF lilimtangaza kuwa kocha bora wa barani hilo msimu wa 2017-2018.

DAR24 TUNAMKARIBISHA KOCHA Zlatko Krmpotic KWA KUSEMA KARIBU SANA KATIKA SOKA LA BONGO, NA TUNAKUTAKIA KILA LA KHERI KATIKA MAJUKUMU YAKO MAPYA UKIWA NA KLABU YA YOUNG AFRICANS.

Kigoma kunufaika na mfuko wa maendeleo wa Kuwait
Video: kuna maisha baada ya uchaguzi - ACP Chatanda