Mwanasiasa mkongwe aliyewahi kushika nyadhifa mbalimbali katika Serikali na Chama cha Mapinduzi – CCM,, Stephen Wasira ameteuliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara.
Wasira ambaye jina lake limewasilishwa mbele ya mkutano mkuu wa CCM unaoendelea jijini Dodoma hii leo Januari 18, 2025, amepitishwa na Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Abdulrahman Kinana aliyestaafu.
Akitangaza matokeo, Spika wa Bunge la Tanzania, Dkt. Tulia Ackson alisema matokeo ya kura jumla ni 1,921, Kura zilizoharibika ni kura 4, Kura halali ni 1,917, Kura za hapana 7 na Kura za ndiyo ni 1,910 na kufanya kupatikana kwa ushindi wa asilimia 99.42.