Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika na mbunge wa Bunda, Stephen Wasira amekanusha ripoti zilizoenea kuwa alimpiga ngumi mwenyeki wa CCM wa Wilaya ya Bunda baada ya kutofautiana katika mchakato wa kura za maoni.

Taarifa hizo zilizoenea kwenye mitandao ya kijamii wiki hii zilieleza kuwa Wasira alishindwa kuvumilia walipokuwa kwenye kikao cha michakato ya kura za maoni, pale alipoghafirishwa na mwenyekiti huyo wa Bunda ngazi ya Wilaya na kuamua kumpiga ngumi.

“Hakuna ukweli hata kidogo…unajua siasa kuna fitina, hilo ni jambo ambalo lilienezwa bila ukweli wowote na tunaintend baada ya kumaliza tutazungumza na waandishi wa habari ili kuwafanya watanzania waelewe ukweli,” Wasira aliiambia E-Fm Radio mapema leo asubuhi.

Hata hivyo, Wasira alimrushia lawama mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mara kuwa chanzo cha taarifa hizo alizoziita za uzushi kwa lengo la kumchafua.

“Tuna-problem hapa na mwenyekiti wa CCM wa mkoa (Mara) ambaye naye ameamua kugombea ubunge hapa, kwa hiyo anajaribu kutumia mbinu hizo chafu kujaribu kuchafua tu jina langu lakini hakuna kitu kama kile,” aliongeza.

Matukio ya kushambuliana yamekuwa yakiripotiwa katika mchakato wa kura za maoni za Chama Cha Mapinduzi zinazoendelea katika maeneo mbalimbali nchini. Hivi karibuni, Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai aliripotiwa kumpiga kwa fimbo hadi kupoteza fahamu mgombea mwenzake, Dkt. Joseph Chilongani.

Wiki kadhaa zilizopita wagombea wengine wa ubunge katika mchakato wa kura za maoni CCM, jimbo la Arusha mjini waliripotiwa kupigana ngumi.

Msimamo wa Viongozi CCM Zanzibar Kwa Lowassa Ni Sauti Ya Maelfu Ya Wanachama?
Liverpool Kumng’oa Young Old Trafford