Utafiti mpya uliotolewa leo Desemba 16,2020 unaonesha idadi kubwa ya watu duniani hawataweza kupata chanjo ya Covid-19 hadi 2022, huku kwa mataifa tajiri kukiwa na uwezekano wa zaidi ya nusu kuipata katika nusu ya kwanza 2021.

Katika kipindi hiki ambacho kumekuwa na matumaini ya chanjo hiyo kuzuia janga hilo ambalo limesababisha vifo takribani watu milioni 1.6, mataifa kama Marekani, Uingereza na Umoja wa Falme za Kiarabu yameanza programu za utoaji wa chanjo kwa watu wake.

Utafiti wa asasi yenye kujikita katika masuala ya afya ya John Hopkins Bloomberg, unaonesha mataifa tajiri ambayo yanafanya jumla ya asilimia 14 ya mataifa duniani yameagiza zaidi ya nusu ya dozi ya chanjo ambayo inatarajiwa kuzalishwa na makampuni 13 hadi mwaka ujao huku kukiwa na mashaka kwa mataifa masikini kuachwa nyuma.

Mataifa mengi yamejiunga na chombo cha ununuzi kinachoratibiwa na shirika la Afya Duniani (WHO) na Umoja wa Uvumbuzi wa kujihami na majanga na muungano wa chanjo GVI kwa lengo la kuhakikisha watu wote wanapata chanjo bila kujali uwezo walionao.

Zidane: Benzema ni mchezaji wa kipekee
JPM: mawaziri na manaibu mmeanza kazi vizuri

Comments

comments