Muigizaji wa kike wa filamu za kiswahili, Wastara Juma amefunga ndoa na mbunge wa Donge, Sadifa Khamis ambaye pia ni mwenyekiti wa Umoja wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa.

Muigizaji huyo ambaye picha ya ndoa yake hiyo ya kimyakimya ilianza kuonekana kwenye mitandao hivi karibuni, alithibitisha kuwa picha hizo ni za tukio la kweli la ndoa yake.

“Kweli nimefunga ndoa jana (alhamisi), Ndoa ni dua tu sherehe ni maamuzi lakini cha umuhimu ni ndoa na imepita salama, tumshukuru Mungu,” Wastara aliiambia Bongo5 jana.

Awali, Wastara aliolewa na muigizaji mwenzake, Sajuki ambaye alifariki Januari 2013 baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Picha: Mchepuko Mpya wa Tyga kutoka Brazil unaomliza Kylie
TFF Yatoa Shukuran Kwa Watanzania Waliompokea Samatta