Kwa mara ya kwanza Serikali ya Sudan imeruhusu sikukuu ya Krismasi kuadhimishwa nchini humo baada ya miaka sabini.

Siku hiyo imesherehekewa na asilimia tatu ya watu ambao ni wakristo nchini humo huku asilimia 97 ya waliobaki ni waislamu.

Kuruhusu mapumziko ya siku ya Krismasi ni miongoni mwa mabadiliko makubwa ambayo yameanza kuonekana baada ya kuingia madarakani kwa kiongozi mpya, kufuatia kuondolewa kwa Rais wa zamani Omar al-Bashir mwezi Aprili.

Waziri anayeshunghulikia masuala ya dini Nasrudin Mufreh, amesema hatua hiyo imekuja baada ya katiba mpya kuruhusu Uhuru wa kuabudu.

Ripoti: Mtandao wa kuuza watoto hatari kama ‘wa unga’, wana mbinu na nguvu
Arusha: Amuua mke wake baada ya kumpikia chai Krismasi