Zaidi ya Wataalam 1,000 wa Afya wakiwemo Mawaziri kutoka Mataifa ya Afrika, wanakutana Botswana kwa mkutano wa kikanda wa Shirika la kimataifa la Afya – WHO kujadili nanma ya kuyakabili majanga na milipuko ya magonjwa mbalimbali.
Akihutubia mkutano huo wa siku tano, Mkuu wa kituo cha kuzuia na kudhibiti magonjwa cha WHO barani Afrika, Jean Kaseya amesema kuna umuhimu wa Afrika kuwa tayari kukabiliana na majanga, hasa baada ya kuonesha mapungufu wakati wa janga la Uviko-19.
Mkuu wa Shirika la Afya Ulimwenguni – WHO, Tedros Ghebreyesus amesema mabadiliko ya hali ya hewa yameongeza uwepo wa changamoto za kiafya na kwamba Afrika ilikuwa na changamoto ya kutoa chanjo wakati janga la Uviko-19.
Wataalam hao, pia wanalenga kuhakikisha kuwa Afrika imejiandaa vilivyo kupambana na majanga yajayo bila kuwa na athari nyingi kama ilivyowahi kutokea katika siku za nyuma.