Wataalamu wa mataifa mbalimbali Barani Afrika, wamezindua utafiti kuhusu uhamaji wa hali ya hewa, huku wakionya kuwa upo uwezekano wa watu milioni 86 kukosa makazi ifikapo 2050 kutokana na mabadiliko hayo.

Wataalam hao, ambao ni wawakilishi wa tume za ushauri wa mashirika ya ushauri wa kiuchumi Afrika, wameyasema hayo wakati wa mkutano unaofanyika jijini Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo – DRC.

Mmoja wa Washiriki, Ahmed Reda Chami kupitia hotuba yake alionya kuwa, “upo uwezekano wa kuwa na Wahamiaji wa ndani hadi milioni 86 ifikapo mwaka 2050 iwapo hakuna hatua zinazochukuliwa kupunguza athari za mabadiliko ya hali ya hewa basi hili tulitarajie.”

Aidha, utafiti huo uliofanywa na Mabaraza ya Kiuchumi na Kijamii na Taasisi Sawa za Afrika – UCESA, unaofadhiliwa na Benki ya Dunia pia utajaribu kutazamia ukubwa wa matatizo kwa siku zijazo na jinsi ya kuyakabili.

Marcon adai Balozi wake alikuwa akinyimwa Chakula Niger
TEHAMA: Kakere ataka maoni chanya maboresho Kidijitali