Timu ya Wataalamu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) imetoka leo kwenye karantini katika mji wa Wuhan nchini China ili kuanza uchunguzi wake wa vyanzo vya virusi vilivyosababisha janga la ugonjwa wa COVID-19.

Watafiti hao, ambao walihitajika kuwa kwenye karantini kwa siku 14 baada ya kuwasili China, wameondoka leo hotelini walimokuwa na haikubainika haraka walikoelekea.

Ujumbe huo wa Wataalamu umegubikwa na siasa, huku China ikilenga kujiondolea lawama kwa tuhuma za kutochukua hatua za mapema kuhusiana na mlipuko wa virusi vya corona.

Mapema mwezi huu, Afisa wa zamani wa WHO Keiji Fukuda, ambaye siyo sehemu ya ujumbe ulioko Wuhan, alitahadharisha dhidi ya kutarajia mafanikio yoyote, akisema inaweza kuchukua miaka kabla ya kufanya mahitimisho yoyote thabiti kuhusu chimbuko la virusi hivyo.

Ikumbukwe kuwa ugonjwa wa virusi vya Corona ulianzia katika mji wa Wuhan nchini China mwishoni mwa mwaka 2019.

Majaliwa ataka wamachinga wakumbukwe
PSG wamng'ang'ania Dele Alli