Bodi ya wataalam wa ununuzi na ugavi ( PSPTB ) imetangaza matokeo ya mtihani wa 23 ya kitaaluma ya Ununuzi na Ugavi ambapo wanafunzi 230 wanatakiwa kujisajili upya wakitarajiwa kurudia tena mtihani huo.

Akitangaza matokeo hayo jijini Dodoma Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) Godfred Mbanyi amesema kuwa jumla ya wadahiliwa walikuwa 479, kati yao waliofanikiwa kufanya mitihani ni 427 ambapo 28 kati yao hawakufanya kabisa mtihani huo.

Ameongeza kuwa katika mitihani mingi ya Bodi inayohusiha maswala ya mahesabu, takwimu, Uchumi na wanafunzi wamekuwa wakifanya vibaya hivyo wanapaswa kuweka juhudi kwa sababu ndio maeneo ambayo watakwenda kufanyia kazi.

Amesema jumla ya Masomo ni 32 na kati ya hayo Masomo 6 wamefanya vibaya sana, 17 ni ufaulu wa Wastani na masomo 11 wamefanya vizuri kiasi na kufanya jumla ya wastani wa ufaulu katika mitihani hiyo ya Bodi ya kataalamu ya Ununuzi na Ugavi kuwa ni asilimia 34.6% kwa mitihani hii ya 23.

Kuanzia Jumatatu ya tarehe 14, march 2022 dirisha litakuwa wazi kwa ajili ya wanafunzi watakaohitaji kufanya mitihani hii ya bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi ambapo fomu za kujiunga zitapatikana katika tovuti ya bodi hivyo usajili wote utafanyikia mtandaoni na kuwataka wanafunzi kujitokeza kwa wingi.

Kisinda aitahadharisha Simba SC
Sudan yajitenga na Dunia; Yaendelea kukuza uhusiano na Urusi