Waziri wa Viwanda na biashara Innocennt Bashungwa ameiagiza tume ya ushindi ya kibiashara na shirikisho la ubora wa viwango (TBS) kufanya msako na kuwachukulia hatua wafanyabiashara watakaobainika kuongeza bei ya vitakasa mikono (sanitizers) pamoja na Barakoa (Mask) kwa lengo la kujipatia faida kubwa katika kipindi hiki kigumu cha mapambano dhidi ya virusi vya Corona.
Agizo hilo limetolewa leo March 21,2020 ambapo pia amewaonya wafanyabiashara walioficha bidhaa kuacha mara moja huku akiwatoa hofu watanzania kuhusu upatikanaji wa bidhaa hizo na kuongeza kuwa serikali inafanya kila linalowezekana kuhakikisha bidhaa zinapatikana kirahisi na kwa bei nafuu.
Aidha watanzania wametakiwa kuwa makini kwa kufuata maelekezo yanayotolewa na wizara ya Afya ili kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona kwa kunawa mikono kila mara na kuachana na mikusanyiko isiyo ya lazima.
Mpaka sasa Tanzania imethibitisha kuwa na wagonjwa 6 wenye maambukizo ya virusi vya Corona, ambapo nchini Italia visa vya ugonjwa huo bado vinaongezeka.