Jimbo la California nchini Marekani limetangaza kugawa zawadi ya pesa kwa watu wanaokubali kuchomwa chanjo ya Covid-19.

Takriban zawadi ya dola milioni 116.5 imetengwa kwa ajili ya kusambazwa katika jimbo la California ili kuhamasisha umma kukubali kupewa chanjo ya corona.

Hayo yameelezwa na Gavana wa California, Gavin Newsom, ambapo katika Jimbo hilo zaidi ya watu milioni 20 wamechomwa chanjo ya corona na watapewa zawadi ya pesa kuanzia Juni 4.

Aidha, Newsom amebainisha kuwa watasambaza jumla ya dola milioni 116.5 kama zawadi itakayojumuisha cheki ya dola milioni 1.5 kwa watu 10, dola 50,000 kwa watu 30 na dola 50 kwa watu milioni 2.

Lengo ni kutoa chanjo kwa asilimia 70 ya idadi ya watu ifikapo katikati ya mwezi Juni ili kupunguza hatua za Covid-19.

Mbali na California, majimbo mengine nchini humo yametenga rasilimali ili kutekeleza mpango huo.

Helikopta ya Raila Odinga yapata ajali
Uhamiaji yalaani kitendo kilichofanywa na Askari wake, yawasimamisha kazi