Wateja wa maeneo yanayouza vilevi katika Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam watalazimika kununua na kwenda navyo majumbani kwao, baada ya Mkuu wa Wilaya hiyo, Sophia Mjema kutangaza marufuku ya watu kukaa bar.

Kupitia tamko lake, Mkuu huyo wa Wilaya amesema kuwa ni marufuku watu kufurika katika maeneo hayo ya starehe, na kwamba mmiliki wa bar atakayekaidi agizo hilo pamoja na watu watakaokusanyika watachukuliwa hatua kali.

Hatua hiyo imekuja ikiwa ni sehemu ya jitihada za kupambana na maambukizi ya covid-19, wakati ambapo Serikali imetangaza kuwa maambukizi yamefikia visa 147 hadi jana, Aprili 17, 2020.

Aidha, baadhi ya sehemu za starehe ikiwa ni pamoja na klabu ya maafuru ya Forty Forty Lounge na Kaitesi zilizoko Tabata jijini humo zimetangaza kusimamisha huduma zake hadi itakapotoa taarifa zaidi.

Serikali imeendelea kuwataka Watanzania kuchukua tahadhari kuepuka mikusanyiko, kuepuka safari zisizo za lazima na kuhakikisha wananawa mikono kwa maji yanayotiririka na sabuni kama sehemu ya kuchukua hatua.

WHO yahofia corona kuim Afrika, yakadiria vifo na ongezeko la umasikini

Mtanzania akutwa na corona Uganda
WHO yahofia corona kuiumiza Afrika, yakadiria vifo na ongezeko la umasikini