Wenyeji katika mji wa Hallstatt nchini Austria wameshiriki katika maandamano ya kupinga utalii wa watu wengi wanaotembelea mji huo wenye zaidi ya wakazi 700 na hupata hadi wageni 10,000.
Wakazi wanatoa wito wa kuweka mipaka kwa idadi ya watalii wa kila siku, na kupiga marufuku mabasi ya watalii baada ya 17:00 saa za ndani ambapo licha ya utalii kuwa mzuri kwa uchumi wa Hallstatt, baadhi ya wenyeji wanasema wageni wamekuwa wengi.
Hallstatt, pamoja na nyumba zake za kupendeza za zamani kwenye ufuo wa ziwa safi la Alpine lililozingirwa na milima , imekuwa sehemu kubwa ya utalii katika miaka ya hivi karibuni.
Mnamo 2006, iliangaziwa katika tamthilia ya kimapenzi ya Korea Kusini – ikikuza umaarufu wake huko Asia – ikiwa na mfano wa mji huo uliojengwa nchini Uchina miaka sita baadaye.