Wakati Azam FC wakitarajiwa kupambana dhidi ya Ruvu Shooting leo Ijumaa (Desemba 18) Uwanja wa Azam Complex Chamazi, baadhi ya wachezaji wa klabu hiyo wataendelea kuwa nje ya kikosi, kwa sababu za kuwa majeruhi.  

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasilino ya Azam FC Zakaria Thabit amesema watawakosa wachezaji watano kwenye mchezo wa leo dhidi ya Ruvu Shootong, hatua mbayo inaendelea kutoa nafasi kwa wachezaji wengine kuziba nafasi zao.

“Tutamkosa mshambuliaji Prince Dube ambaye aliumia kwenye mchezo dhidi ya Young Africans, Salim Abubakar,’Sure Boy’, aliumia kwenye mchezo dhidi ya Biashara United Mara, Richard Djod aliumia kwenye mchezo dhidi ya Namungo FC, Abdalah Sebo aliumia kwenye mchezo dhidi ya Biashara United na Bryson Raphael aliumia kwenye mchezo dhidi ya Namungo FC.” Amesema Thabit Zakaria.

Mshambuliaji Prince Dube.

Hata hivyo Thabit ameongeza kuwa wachezaji Bryson na Djod wanasubiri ripoti ya kuweza kujua hali zao kama wanaweza kuwa sehemu ya kikosi, lakini mpaka sasa wapo kwenye orodha ya walio majeruhi.

Azam FC inayoshika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu kwa kuwa na alama 28, na Ruvu Shooting wapo katika nafasi ya nne kwa kua na alama 24.

Young Africans wanaendelea kuongoza msimamo huo kwa kumiliki alama 37, wakifuatiwa na wapinzani wao katika soka la Bongo Wekundi wa Msimbazi Simba wenye alama 32.

Polisi walivyozima sherehe ya ufuska Dar
DPP awakazia waliowekeza Qnet