Watu watano wamefikishwa mahakamani kwa tuhuma za kujaribu kumuua kwa bomu Waziri Mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed katika mkutano wa kampeni uliofanyika Juni mwaka huu.

Shambulio hilo la bomu lililomlenga Waziri Mkuu huyo lilisababisha vifo vya watu wawili na kujeruhi zaidi ya watu 100, lakini Abiy hakupata madhara.

Hata hivyo, baada ya kusomewa mashtaka hayo leo na mwendesha mashtaka wa Serikali, watuhumiwa hao hawakutakiwa kujibu tuhuma hizo mbele ya mahakama hadi upelelezi utakapokamilika.

Waziri Mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed

Waziri Mkuu huyo aliondolewa haraka kwenye eneo hilo, na Serikali ililitaja tukio hilo kama jaribio la kumuua kiongozi wa Serikali ambalo halikufanikiwa.

Kwa mujibu wa maelezo ya mashtaka, bomu hilo lililipuliwa Juni 23 ambapo maelfu walikuwa wamehudhuria mkutano wa hadhara jijini Addis Ababa wakimuunga mkono Waziri Mkuu Abiy.

Gavana anayetuhumiwa kumuua mpenzi wake akwama selo
Serikali yanunua mashine mpya ya kutoa tiba ya mionzi