Jeshi la Polisi mkoani Dodoma linawashikilia watu watano kwa tuhuma za mauaji ya mwalimu Eradius Lucas Mgaya mkazi wa kijiji cha Chilungulu.

Kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto amebainisha hayo jana wakati akiongea na waandishi wa habari jijini Dododma.

Amesema tukio hilo lilitokea Aprili 7 mwaka huu ambapo inadaiwa kuwa watuhumiwa hao walimpiga marehemu na kitu chenye ncha kali na kumtupa kwenye shamba la shule baada ya kumvizia njiani wakati akirejea nyumbani kwake.

” Bado tunaendelea kufanya uchunguzi kuhusiana na tukio la kifo cha Mwalimu Godfrey na tunaendelea kuwashikilia watuhumiwa wa mauaji hadi hapo uchunguzi utakapo kamilika” Amesema kamanda Muroto.

Adha katika hatua nyingine Kamanda Muroto amesema jeshi la polisi linamshikilia Godfrey Shirima (22) ambaye ni mpiga picha mkazi wa Dodoma akiwa na silaha aina ya bastola yenye namba za usajili 016975 akimiliki kinyume na sheria ambapo amekutwa akitumia katika matukio ya uhalifu.

Video: Ndoo 200 zakusanywa soko la Mwananyamala Vita vya Corona
TMA yatahadharisha mvua kubwa kwa mikoa 7