Wafanyabiashara watano waliobainika kukwepa kodi katika sakata la upotevu wa makontena 349 waliopewa siku saba na Rais John Magufuli kujisalimisha na kulipa kodi hiyo wamekataa kutii amri hiyo.

Hayo yamebainishwa jana na Kaimu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato nchini (TRA), Alphayo Kidata alipokuwa akitoa taarifa ya ukusanyaji wa mapato katika mwezi Desemba ambayo ilionesha kuvuka malengo yaliyowekwa.

“Wafanyabiashara watano bado hawajalipa kodi ya kontena zenye gharama ya shilingi bilioni mbili. Hatua za kisheria zinaendelea kuchukuliwa dhidi yao baada ya kuisha muda wa msamaha wa rais,” alisema Kidata.

Alieleza kuwa wafanyabiashara 38 ambao waliondoa makontena bandarini kinyume cha taratibu za forodha na hivyo kukwepa kodi walilipa walilipa shilingi bilioni 11.8.

 

Zinedine Zidane: Hapa Kazi Tu
Siku ya Magufuli Kupewa Rungu la CCM Yabainika, Wajumbe Wagawanyika