Klabu ya Ihefu FC imetangaza kuachana Rasmi na Wachezaji watano katika kipindi hiki cha Dirisha Dogo la Usajili, ili kupisha usajili wa Wachezaji wengine ambao wataongeza nguvu kwenye kikosi cha Klabu hiyo.
Ihefu FC imetangaza majina ya wachezaji hao kwa mujibu wa Kanuni za usajili, huku ikiamini watakaoingia kupitia Dirisha Dogo la Usajili, watakuwa na Sifa za kuhakikisha timu yao inasalia Ligi Kuu Tanzania Bara kwa msimu ujao wa 2023/24.
Kwa mujibu wa Kurasa za Mitandao ya Kijamii za Klabu hiyo ya Wilayani MBarali mkoani Mbeya, Wachezaji walioachwa Klabuni hapo ni Kinyozi, Ally Oviedo, Sadick, Mujwaguki na Omary.
Sababu kubwa ya kuachwa kwa wachezaji hao ni kushindwa kufikia kiwango kinacholishawisho Benchi la Ufundi linaloongozwa Kocha mzawa Juma Mwambusi kwa kusaidiana na Zubeir Katwila.
Ujumbe ulioambatana na taarifa za kuachwa kwa wachezaji hao umesomeka: THANK YOU….⚽️??
Asanteni kwa kuwa nasi na Asanteni kazi yenu ya kuipambania klabu yetu kwa Muda wote mliokuwa ndani ya MbogoMaji.
Tunawatakia kheri katika maisha mengine ya soka popote Muendako.