Klabu ya Mtibwa Sugar imetangaza kusajili wachezaji wapya watano kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara, huku ikipandisha wachezaji wawili vijana chini ya miaka 20.
Msemaji wa klabu hiyo, Thobias Kifaru amesema kuwa wanaamini wamesajili wachezaji ambao wataleta kwenye kikosi hicho hasa baada ya kutofanya vema kwa misimu kadhaa.
“Tulikaa chini na kuangalia aina gani ya usajili ambao tunatakiwa kufanya ili ka daraja,” amesema Kifaru.
Taarifa iliyotolea na klabu hiyo ambayo ilitwaa Ubingwa wa Tanzania Bara mwaka 1999 na 2000, imewataja wachezaji waliosajiliwa kuwa ni Fredrick Magata kutoka Mbeya Kwanza, Abdul Hillary Hassan kutoka KMC, Juma Luzio ambaye amerejea tena kwenye kikosi hicho, Kassim Shaaban Haruna aliyekuwa akiichezea Polisi Tanzania, Abalkassim Suleiman na Kevin Nashon kutoka Singida Fountain Gate FC.
Mbali na wachezaji hao, Mtibwa Sugar pia imewapandisha wachezaji Omari Ally Marungu na Said Kazi ambao walikuwa kwenye kikosi cha timu hiyo kilichotwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Vijana chini ya miaka 20 hivi karibuni, michuano iliyofanyika kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es salaam. Marungu na Kazi ni kati ya wachezaji waliofunga mabao na kufanya vema kiasi cha kuingoza timu hiyo kuwa mabingwa.
Hata hivyo, Mtibwa ilimpoteza Mshambuliaji wake tegemezi ambaye alikuwa mfungaji bora wa ligi hiyo chini ya miaka 20, Athumani Masumbuko ‘Makambo’ ambaye baada ya kumalizika tu alinyakuliwa na Mashjajaa FC.