Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Innocent Bashungwa amewasimamisha kazi Maafisa watano Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Mkoani Manyara, ili kupisha uchunguzi kwa kuisababishia hasara Halmashauri na matumizi mabaya ya madaraka.
Bashungwa, amechukua uamuzi huo Septemba 27, 2020 wakati akifanya majumuisho wa ziara ya kikazi ya kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu, Halmashauri ya Wilaya ya Hanang’ na Halmashauri ya Mji Mbulu, mkoani Manyara.
Amesema, Julai 12, 2022 aliyekuwa anakaimu ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya Mbulu, David Ali Assey aliandika barua kwa Kampuni binafsi ya kukopa kiasi cha shilingi milioni sita laki saba kwa aijli ya matumizi ya ofisi na kuelekeza fedha hiyo kuwekwa kwenye akaunti binafsi ya Davidi ali Assey ambaye ni Mhasibu wa Halmashauri.
Amesema, Taarifa ya CAG ya ukaguzi wa kawaida kwa mwaka wa fedha wa 2020/21 ilielekeza Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Manunuzi, Juma Ibrahim Mvumo achukuliwe hatua stahiki kwa kushindwa kuandaa vyema masharti ya zabuni na tangazo lake pamoja na kutofanya ufuatiliaji na uhakiki wa uhalali wa kampuni ya M/S Dicsamo Traders General Supplies Co. Ltd.
Bashungwa amesema aliyekuwa Kaimu Mweka Hazina, Ramadhani Mwakamyanda na weka Hazina wa sasa, Respicius Kagaruki wachukuliwe hatua kwa kulipa gharama za uwakala kwenye akaunti ya binafsi badala ya akaunti ya kampuni M/S Dicsamo Traders iliyopewa zabuni ya kukusanya mapato ndani ya Halmashauri kiasi cha Shilingi 188,499,328.
Watumishi hao, ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Manunuzi, Juma Ibarahim Mavumo, aliyekuwa Kaimu mweka hazina, Ramadhani Mwakamyanda, Mweka hazina wa sasa, Respicius Kagaruki, Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA, Nyanda Komanya Msirikale na Mhasibu wa Mapato, David Assey.