Baada ya sampuli 1,116 kupimwa ndani ya saa 24 zilizopita, Uganda imetangaza wagonjwa wapya 31 wa covid -19 waliopatikana na kufanya jumla ya maambukizi kufikia 253.
Wizara ya Afya nchini humo imesema kati ya wagonjwa 23 waliopatikana mipakani, 20 ni madereva wa malori ambapo 16 ni Watanzania na 4 ni Wakenya. Wote wamekabidhiwa kwa nchi zao.
Wagonjwa 23 wa kutoka mipakani wamepatikana baada ya sampuli 896 kuchukuliwa na 8 ni walipimwa wakiwa Karantini baada ya kukutana na madereva waliotangazwa awali kuwa na virusi vya corona.
Aidha, Wizara imebainisha kuwa hadi kufikia sasa jumla ya Wagonjwa 69 wamepona na hamna kifo.