Watanzania 27 wamekamatwa Mombasa nchini Kenya baada ya kuingia nchini humo bila vibali maalum vya kufanyakazi

Mamlaka ya usalama nchini Kenya inaendelea na mipango ya kuwarejesha nchini kwao Watanzania hao ambao hawakufuata utaratibu wa kuingia nchini humo.

Aidha, baadhi ya watu hao wameshikiliwa na polisi katika kituo cha Likoni wakati wakisubiri kurejeshwa nyumbani Tanzania ili waweze kufuata taratibu husika za nchi.

Kamanda wa Polisi wa mji wa Mombasa, Johston Ipara ameeleza kwamba Watanzania hao ni miongoni mwa wahamiaji wengine kutoka katika nchi za Congo, Somalia, Eritrea na Ethiopia ambao walikamatwa kwa kutokuwa na vibali vya kusafiria.

Hata hivyo, ingawa raia wa nchi za Afrika Mashariki wanauwezo wa kutumia kitambulisho cha taifa kuweza kuingia na kutoka katika nchi zote tano za Afrika Mashariki ikiwa ni pamoja na Kenya, Burundi ,Rwanda,Tanzania na Uganda raia hao inasemekana hawakuwa na kitambulisho cha taifa wanalotoka.

 

Video: Ukatili wakutisha Dar mgambo wa makonda, CCM yawatosa wasanii kampeni 2020
Makonda: Ninalaani tukio la kushambuliwa raia kisa 50,000 ya usafi