Jumla ya Watu 11 kutoka nchi za Tanzania, Pakistani na Iran wamehukumiwa kifungo kwa kushiriki kusafirisha Dawa za Kulevya aina ya heroin nchini Marekani.

Watanzania waliohukumiwa ni Ali Khatib Haji Hassan (49), Makame Haji Mwinyi (49), Ernest Michael Mbwile (35), Abdulahtif Juma Maalim (43), Ibrahim Omary Madega (52), Tiko Emanuel Adam (41), Iddy Saleme Mfullu (46), Mohammed Said Mohammed (48) na Daud Michael Vedasto (58)

Wengine ni Salim Omar Balouch (36) kutoka Iran na Abdul Basit Jahangir (40) kutoka Karachi, Pakistan ambapo wote walihukumiwa Agosti 07, 2019 baada ya Jaji kusikiliza shauri lao kwa siku mbili mfululizo

Aidha, Jahangir amehukumiwa kifungo cha miezi 151, Mfullu na Mohammed wamehukumiwa kifungo cha miezi 50 kila mmoja huku Hassan akihukumiwa miezi 99, Mwinyi miezi 62, Mbwile miezi 52, Maalim miezi 46, Madega miezi 87, Adam miezi 37 na Vedasto miezi 46

Aidha, Mahakama imemuhukumu Balouch kifungo cha miezi 135 huku ikisema kuwa raia ambao si wa Marekani wanatarajiwa kusafirishwa kurudishwa nchini kwao baada ya hukumu hiyo.

Video: Watu zaidi ya 57 wafariki dunia mkoani Morogoro
VIDEO: Hatima ya Lissu kurejea kujulikana Agosti 20, Kikwete asimulia siri ya kuanzishwa kwa SADC