Bilionea anayemiliki kampuni kubwa ya Mohammed Enterprises nchini (MeTL), Mohammed Dewji `Mo’ amewataka vijana kuacha kulalamika bali wafanye maamuzi magumu ndani ya mwaka 2018 yatakayowaletea maendeleo.

Dewji ametoa ujumbe wake huo kupitia mitandao yake ya kijamii amewasihi Watanzania kama wanaona hawapendezwi na kitu fulani njia nzuri ni kukibadili kitu hicho na kuacha kulalamika kwani hakutaweza kubadili jambo lolote lile.

“Kama hupendi kitu fulani, (jaribu) kibadilishe! Unataka kupunguza uzito? Badilisha milo yako, fanya mazoezi. Unataka kukutana na watu wapya? Toka nje, tembea na jichanganye na watu wengine! Kumbuka kulalamika hakubadilishia jambo usilolipenda!,”ameandika Dewji

 

 

Msigwa awapongeza Askofu Kakobe na Gwajima
LUkuvi: Utambuzi wa umiliki wa maeneo na urasimishaji ni endelevu kwa mikoa yote nchini