Chuo Kikuu cha Jimbo la St. Petersburg cha nchini Urusi kimetoa ofa maalum kwa Watanzania walipo nchini Urusi wanaotaka kujifunza lugha hiyo bila malipo, wakilenga kuendeleza uhusiano wa kibiashara na uchumi na hatua inayoongeza nafasi za kwa pande hizo mbili za raia wake kufanya kazi upande wowote.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na chuo hicho imeeleza kuwa, programu hiyo inayoratibiwa na Wizara ya Elimu nchini Urusi, ni maalum kwa Watanzania watakaopata nafasi ya kusoma nchini humo, ambapo watajifunza pia na lugha hiyo.

Chuo hicho kikongwe zaidi nchini Urusi, pia kimekuwa kikitoa programu mbalimbali za kielimu na kitamaduni na mafunzo amabayo yanaruhusu kujua vizuri lugha ya Kirusi kutoka mwanzo.

Aidha, Agosti 15 – 16, 2023 lilifanyika tamasha la Utamaduni wa Kirusi katika kituo cha utamaduni cha Urusi jijini Dar es Salaam, ambapo washiriki zaidi 200 walihudhuria.

Aidha, kupitia tamasha hilo walijionea tamadani mbalimbali za Kirusi ikiwemo mikate, ngoma na kufundishwa namna ya kusaini kadi za posta za Kirusi kutoka kwa mtaalamu Khokhloma.

Hata hivyo, Walimu wanaofundisha lugha ya Kirusi kwa wakazi wa Tanzania wanaweza kutumia fursa za Kituo hicho kwa mafunzo ya kitaaluma.,Mihadhara na semina kutoka kwa wataalam wakuu kutoka Chuo Kikuu cha St Petersburg na vyuo vikuu vingine vya Urusi, zitafanyika mnamo Agosti 27 – 28, 2023 kwa Walimu.

BRICS yatupiwa lawama ukoloni mamboleo
Azam FC kulipa kisasi Azam Complex