Waziri ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe, amewataka Watanzania wasiwe na hofu kwani Serikali inafanya juhudi kubwa za kuikomboa ndege ya ATCL iliyoshikiliwa nchini Afrika Kusini.

Waziri Kamwelwe ameyasema hayo leo Septemba 3, 2019, wakati wa uzinduzi wa Mkutano wa Kimataifa wa Shirikisho la Kimataifa la watoa huduma za Anga na Uongozaji Ndege (CANSO).

“Ndio maana hata lilipotokea tatizo la ndege yetu, kwakweli niwashukuru watanzania hata wajukuu zangu sijui aliwaambia nani walikuwa wananiuliza babu ndege iko wapi, nikashaangaa kumbe na wao wanalijua hili, nikawaambia tulieni inarudi, hata waandishi wa habari ndio maana nimekataa msinihoji tunaheshimiana na nyinyi mnahaki ya kuuliza lakini kwa juhudi kubwa zinazofanyika itarudi tu,”amesema Waziri Kamwelwe.

Ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) ilishikiliwa nchini Afrika ya Kusini Agosti 24, 2019, kwa amri ya Mahakama nchini humo, kutokana na kesi iliyofunguliwa na raia mmoja wa huko,

 

Benki zatakiwa kuboresha huduma kuvutia taasisi za umma
Wolper acharuka warembo bongo movie kutumika kingono na waandaaji