Serikali imeanza kuchukua hatua za kuwarejesha nchini Watanzania takribani 300 waliopo nchini Ukraine kutokana na hali ya usalama kuendelea kuzorota nchini humo.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Emmanuel Buhohela amesema katika taarifa leo, Feb. 27 kuwa hatua zinazoendelea kuchukuliwa ni pamoja na kuwaondoa hadi nchi jirani za Polandi na Romania ambako kuna utulivu.

“Hatua hii itatoa fursa kuwawezesha raia wetu kurejea nchini kwa usalama,” amesema Buhohela katika taarifa kwa vyombo vya habari.

Hatahivyo, serikali imesema hadi sasa hakuna Mtanzania aliyepata madhara kutokana na kile kinachoendelea Ukraine.

Athari zitokanozo na ulaji wa udongo
Waziri Jafo atoa siku 14 tatizo hili lipatiwe ufumbuzi