Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi – CCM, Richard Kasesela amesema hadhani kama baadhi ya Watanzania wanafahamu umuhimu wa Mazingira, huku akiwafananisha waharibifu wa mazingira kama watu wanaokata tawi waliklokalia.

Kasesela, aliyasema hayo wakati akihojiwa na Dar24 Media nyumbani kwake Mjini Iringa kuhusu mapambano ya Wadau wa Uhifadhi, Mazingira na utunzaji wa vyanzo vya maji wanavyohaha kuhakikisha suala hilo.

Amesema, “bado sidhani kama wananchi wote wanauelewa juu ya masuala ya uhifadhi na utunzaji wa mazingira bado elimu inahitajika ili watambue kwamba Mazingira yana maana kubwa kwao maana anayeharibu Mazingira naye anaathirika sasa kama akilijua hili hataweza fanya hivyo.”

Kuhusu uhusika wa siasa na suala la Mazingira, Kasesela ambaye pia aliwahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Iringa, amesema vinahusiana moja kwa moja kwakua hata Imani ya CCM inatambua na imeanisha mambo mbalimbali katika masuala ya uhifadhi na utunzaji wa mazingira.

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Juni 25, 2023
Uasi wa Wagner: Urusi hatarini kukumbwa na machafuko