Licha ya watanzania kufanya shughuli mbalimbali ili kujitafutia kipatao na kuinuka kiuchumi, lakini katika sekta ya kilimo nchini inaelezwa kuwa kwa sasa kilimo kimebadilika huku wakulima wakijihusisha zaidi katika kilimo cha biashara ili kuyafikia maendeleo.

Leonard Sapula ni mtafiti kutoka taasisi ya utafiti wa kilimo Tanzania iliyopo Uyole mkoani Mbeya, amebainisha hayo wakati akizungumza na dar24 mara baada ya mkutano na wataalamu wa kilimo kutoka mikoa ya Iringa, Njombe na Ruvuma uliofanyika katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Njombe mkoani humo.

“kuna mwamko mkubwa sana sasa tofauti na zamani na ukiangalia vikundi vya wakulima ni vingi sana, tofauti na zamani mkulima analima peke yake, anatafuta soko peke yake lakini kutokana na ushirika washirika watano au kumi wanaweza kujaza gari peke yao, kwa hiyo kilimo kimebadilika japo bado hakijafika pale tunapopataka”amesema Sapula

Stela Lwiza ni mtaalamu kutoka shirika la AGRA, waandaaji wa mafunzo hayo kwa maafisa ugani, amesema lengo kubwa la mafunzo yaliyotolewa ni kuwa na uelewa juu ya wadau wa maendeleo wanaofanya shughuli katika maeneo yao ili kuona namna ya utekelezaji wa maendeleo katika mikoa hiyo.

“lengo la kuwakutanisha maafisa ugani hawa ni kuweza kusikia kutoka kwao ni wadau gani walio nao ili kuelewa ni mdau yupi na anatekeleza kitu gani ili kushirikiana kwa pamoja katika utekelezaji wa maendeleo” amesema Stela Lwiza

Baadhi ya wataalamu wa kilimo walio hudhuria katika semina hiyo wamesema kuwa taasisi mbalimbali katika sekta ya kilimo hususani vijijini zina mchango mkubwa huku wengine wakitoa wito kwa mashirika binafsi kuwa wazi katika shuguli zao .

 

Gumzo laibuka ziara ya Rais Trump London
Sababu, madhara ya kukosa choo 'Constipation'