Afisa Mtendaji Mkuu wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC Barbara Gonzalez amewahimiza Watanzania wanaoishi Afrika Kusini kufika Uwanja wa Orlando Kesho Jumapili (April 24), kwa ajili ya kuipa nguvu timu yao.

Simba SC kesho itakua na kibarua kizito cha kuikabili Orlando Pirates ugenini, huku ikiwa na mtaji wa ushindi wa bao moja, walioupata nyumbani Uwanja wa Benjamin Mkapa Jumapili (April 17).

Barbara amesema kikosi cha Simba SC kinaendelea vizuri baada ya kuwasili mjini Johannesburg jana Ijumaa (April 22) na leo Jumamosi (April 23) kitafanya mazoezi ya mwisho katika Uwanja wa Orlando, ambao utatumika kesho Jumapili (April 24) kwa ajili ya mchezo wa Mkondo wa Pili wa Robo Fainali.

Barbara amesema kutokana na uzito wa mchezo huo, watanzania wanaoishi mjini Johannesburg na maeneo ya karibu wanapaswa kufiwa Uwanja wa Oralando kwa ajili ya kuipa nguvu timu ya Simba SC, yenye jukumu la kuiwakilisha nchi yao Kimataifa.

“Tumefika, tunajiandaa, tuko vitani na tunashinda Jumapili,”

“Watanzania wanaoishi hapa Johannesburg wanapaswa kuwa pamoja na sisi  wakati wote, wafike Uwanjani kesho Jumapili ili kuipa nguvu timu ya Simba ambayo ina jukumu kubwa la kuiwakilisha nchi Kimataifa.”

“Wachezaji na hata sisi viongozi tutajihisi furaha endapo watanzania watajitokeza kwa wingi Uwanjani na kuishangilia timu ya Simba SC wakati wote.” Amesema Barbara

Katika mchezo huo Orlando Pirates itapaswa kusaka ushindi wa mabao mawili ama zaidi ili kujihakikishai nafasi ya kutinga Nusu Fainali Kombe la Shirikisho Barani Afrika, huku Simba SC ikipaswa kupambana kusaka ushindi wowote ama kulinda ushindi walioupata Dar es salaam wa bao 1-0.

Orlando Pirates yatamba kuisambaratisha Simba SC
Balozi Milanzi awatuliza wachezaji Simba SC