Baada ya Serikali kutoa agizo kwa wasafiri wote wanaoingia Tanzania kukaa karantini kwa siku 14 kwa gharama zao wenyewe ili kuzuia maambukizi mapya ya virusi vya covid 19 nchini, wasafiri waliowasili wametoa vilio vyao juu ya gharama za hoteli walizopangiwa kukaa karantini.
Malalamiko hayo yametolewa na abiria hao waliowasili nchini kwa kurekodi kipande kifupi cha video akiongea mwanamke mmoja na kutaja hoteli ambazo wamepangiwa kukaa ambazo kwao wameshindwa kumudu gharama.
” hoteli walizotutajia ni Peacock hotel, Rungwe, southern sands, dar palace, hizi ni hoteli ambazo ni ghali Mh. Rais, Waziri mkuu na Mh, Waziri Ummy, hatuwezi ku ‘afford’ kulipia hizi hoteli kwa siku 14″ amesema mama huyo.
Daraja tata la Morogoro laua watano, wazazi wa watoto hawajafahamika
Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu kwa kupitia ukurasa wake wa Instagram amethibitisha kupokea malalamiko hayo na kuwataka wakuu wa mikoa na wilaya kubainisha hoteli ambazo wasafiri wengi watamudu gharama.
” Tumepokea hii changamoto ya sehemu zilizobainishwa kwaajili ya 14 – days mandatory isolation kwa wasafiri waliotoka nchi zilizoathirika zaidi na covid 19. Nawaelekeza ma RC/DC wa mikoa yote kubainisha hoteli / sehemu ambazo wasafiri wengi watamudu” amesema waziri Ummy.
Avunja ukuta na kuiba kichanga cha wiki mbili
Mapema leo wakati wa ziara yake mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amesema maeneo waliyoyatenga kwaajili ya watakao kaa karantini yapo katika ngazi mbalimbali kuanzia gharama ya juu hadi ya chini kabisa kwenye ‘hostels’.