Kufuatia kuendelea kuzorota kwa hali ya usalama nchini Israel na maeneo mengine ya jirani, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeandaa mpango wa kuwarejesha nchini Watanzania waliopo nchini humo na maeneo mengine ya karibu.

Serikali Nchini imesema imefikia uamuzi huo baada ya kufanya tathmini na kujiridhisha kwamba mazingira ya sasa yanaruhusu zoezi hilo kufanyika.

Hivyo, Watanzania walio tayari kurejea nyumbani
wanashauriwa kujiandikisha kwenye Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania uliopo Tel Aviv, Israel kupitia barua pepe: telaviv@nje.go.tz au simu namba: +972 533 044 978 na +972 507 650 072, kabla ya tarehe 15 Oktoba 2023, saa 6 usiku.

Janga jipya Chelsea, Mashabiki wang'aka
Fiston Mayele achekelea kupangwa Kundi F