Jamii ya Kitanzania, imetajwa kuwa na watu wenye busara na wanaoheshimiana ambao hupenda kujadili mambo kwa hoja, na kwamba suala la Bandari halitakiwi kuwagawa kwani Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma – PIC, ilipata maoni mengi kutoka kwa Watanzania na wasomi.
Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa Kamati za Kudumu ya Bunge na Mbunge wa Ukonga, Jerry Silaa amesema wakati akizungumzia upotoshaji unaoendelea kuhusu Mkataba wa uendeshaji wa Bandari, kati ya Serikali ya Tanzania na Dubai.
Amesema, “maoni mengi yanahusika zaidi na mikataba ya utekelezaji na yamepelekwa serikalini yazingatiwe kwenye uaandaaji wa mikataba hiyo. Na Mheshimiwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema maeneo yote hayo yatazingatiwa.”
“Wanaofoka ndio wanaonufaika. Wanaweza kulipwa kwa sababu walikuwa wanachelewesha utendaji wa bandari. Nafasi ya kuhifadhi mizigo bandarini ni mdogo, hivyo mifumo ya ICD hawawezi kufurahia ufanisi wa bandarini chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa sababu huko nyuma walikuwa wananuifaika,” amefafanua Jerry Silaa.