Mtanzania yeyote mwenye kuona kuna eneo anahitaji lifanyiwe marekebisho kwenye mkataba wa IGA, ipo ibara inayosimamia marekebisho ambayo inaruhusu pande zote mbili kutaka wakae na wakafanya marekebisho kwani Watanzani awote wana haki ya kuzungumza.
Hayo yamebainishwa hii leo Julai 28, 2023 na Mbunge wa Ukonga Jerry Silaa na kusema Watanzania wamejitengenezea mazingira ya uoga na ni lazima kujiuliza kipi hatuna nchini na kwamba Tanzania ina haki ya kutaifisha mradi.
Amesema, “na kama pande mbili zitakaa tena kuongeza muda wa majadiliano basi haki itabaki chini ya serikali kwa kuamua namna gani jambo hili linapaswa kutekelezwa, Watanzania wote wana haki ya kuzungumzia mkataba huu, lakini lazima tuuweke kisheria.”
Silaa ameongeza kuwa, “Tanzania tumejitengenezea mazingira ya kujiweka kwenye uoga na kuna mambo tunasema sana, tuna mbuga, tuna ardhi, tuna mlima lakini vilevile ifike wakati tujiulize hatuna nini? Hatuna nini na lenyewe ni swali.”