Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko amesema watanzania wanataka umeme na hivyo kuwataka Viongozi na Wafanyakazi wa Shirika la Umeme Tanzania TANESCO kufanya kila jitihada za kuhakikisha kunakuwa na Nishati ya uhakika.

Biteko ameyasema hayo jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na Wafanyakazi wa Shirika hilo na kuongeza kuwa zinahitajika jitihada za dhati za kuhakikisha kunakuwa na rasilimali watu ya kutosha pamoja na mahusiano mazuri kazini hatua ambayo itaboresha utendaji kazi wa shirika hilo.

Amesema, “Watanzania wanataka umeme, hata tungekuwa na mipango ya namna gani watanzania wanachotaka ni umeme, unaweza kusema fulani anafanya hivi, au mchakato wa kupata rasilimali fedha kwa ajili ya kunua kifaa fulani unaenda hivi lakini watanzania hayo hawayajui, wao wanamjua TANESCO ndio mleta umeme.”

Hata hivyo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba amemuhakikishia Dkt. Biteko kuwa Wizara yake kupitia shirika la TANESCO inafanya kila jitihada za kuhakikisha watanzania wanapata huduma bora na za uhakika za Nishati ya Umeme.

Waliofariki kwa mafuriko Libya wafikia 6,000
DC. Ludewa azindua azindua Kituo cha Afya Mundindi