Lydia MollelĀ – Morogoro.

Waziri wa viwanda na biashara, Dkt. Ashatu Kijaji amewataka Watanzania hasa Wafanyabiashara kuchukua tahadhari kufuatia kuibuka wimbi la utapeli, uwepo wa Makampuni ya Wakala wanaotoa matangazo wakidai kuandaa safari za kibiashara nje ya nchi na kuwalaghai kutoa kiasi cha fedha kama sehemu ya usajili, ili kuweza kushiriki.

Dkt. Kijaji ameyasema hayo wakati alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari Mkoani Morogoro, wakati wa kikao kilicholenga kuwasilisha mwenendo wa bei ya bidhaa muhimu nchini, waziri Ashatu amesema kuwa kuna baadhi ya watu wamekuwa wakitoa taarifa baada ya kutapeliwa.

Amesema, Wakulima wanatakiwa kuhifadhi mazao yao kwa ajili ya chakula kwani uwepo wa uhitaji wa mazao sokoni ni mkubwa jambo ambalo linaweza kusababisha ukosefu wa chakula au kununua mazao hayo waliyoyauza kwa garama kubwa.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Adam Malima amesema wapo wafanyabiashara ambao wanadhulumiwa haki yao, kwa kudanganywa malipo ya bei ya bidhaa tofauti na zile zilizoelekezwa na mamlaka husika.

Hata hivyo, Katika hatua nyingine Serikali imeiagiza tume ya ushindani wa viwanda na biashara kuzunguka kwenye mikoa ya pembezoni, ili kuona ni kwanini bei ya saruji ipo juu licha ya kuwepo kwa changamoto ya Nishati ya Mafuta katika Mkoa wa Kagera na mwanza.

Watafiti wapimwe kwa ubora wa kazi zao - Prof. Mkenda
PSG yajipanga kuibomoa Real Madrid