Raia watatu kati ya wanne kutoka Tanzania wanashikiliwa nchini Kenya baada ya kushindwa kulipa faini ya zaidi ya Shilingi za kitanzania Milioni 2.1 kwa kosa la kuingia nchini humo bila kibali na kutovaa barakoa.

Watanzania hao ambao ni Wafanyabiashara walitozwa Tsh. 600,000 kila mmoja kwa kosa la kutokuwa na vibali na Tsh. 100,000 kwa kutovaa barakoa kama taratibu za Kenya zinavyoelekeza.

Kati ya wafanyabiashara wanne waliokamatwa Novemba 11 walipokwenda kununua nyanya, ni Wilfred Moshi pekee ndiye amefanikiwa kulipa faini baada ya kuchangiwa na ndugu zake.

Kamishna Msaidizi wa Idara ya Uhamiaji mkoa wa Kilimanjaro, Edward Mwenda amethibititisha kushikkiliwa kwa watanzania hao na amesema, wanafanya mawasiliano na Kenya kuona kama Mahakama inaweza kuwasaidia kupunguza faini hizo.

Naibu Kamishna Kidavashari afariki Dunia
Mkurugenzi Jamii Forums ahukumiwa