Watanzania wanaocheza soka katika timu LLC men’s Soccer, Adolf Bitegeko na Daudi Aboud wameiwezesha timu yao kutwaa kombe la Golden Valley Conference nchini Marekani.

Ubingwa huo ambao wameuchukua bila kupoteza mechi hata moja umefanya kuingia kwemye State Playoff ambayo itachezwa kwa mfumo wa mchujo huku ikijumuisha timu kutoka majimbo tofauti tofauti.

“Kilichopo ni kuendelea kuipigania timu yetu katika hatua ya State ambapo kama tutafanya vizuri basi tutakuwa tumepiga hatua kubwa ya kuchukua ubingwa kwa upande wa vyuo,”amesema Adolf.

Hata hivyo, ameongeza kuwa wanaimani kubwa na timu kwani wanauhaka watafanyari katika mashindano hayo kwa kulitwaa kombe hilo na kuleta mapinduzi ya mpira nchini humo.

Magazeti ya Tanzania leo Novemba 13, 2017
Mawakili wa Kenyatta kutinga mahakamani kesho