Watu Watatu wamefariki dunia na wengine watatu kujeruhiwa baada ya kufukiwa na kifusi katika machimbo ya moramu yaliyopo eneo la Kisongo mkoani Arusha.

Akizungmza na Dar24Media Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Salum Hamduni amesema kuwa Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Jeshi la uokoaji na wataalamu wa madini wameunda timu ya pamoja ya kufanya ukaguzi hata wa migodi mingine ili kuhakikisha hali ya usalama lakini pia kuandaa miongozo itakayowasaidia wachimbaji na kuepukana na ajali kama hizo.

“Wenzetu wataalamu hususani wa madini wanaiangalia hali kuna vitu wanatupendekezea ili kuweza kuvifanyia kazi kwa hali ya usalama zaidi kuchimba bila kuleta shida,” amesema Kamanda Hamduni.

Aidha majeruhi walipelekwa katika Hospitali ya Kisongo kwa ajili ya matibabu na mpaka sasa majeruhi wanaendelea vizuri na wote wameruhusiwa.

Eneo hilo la machimbo ya moramu la Kisongo lina wachimbaji zaidi ya mia tano.

Jafo aagiza kukamatwa Mkurugenzi aliyetelekeza makontena
Mchezo wa bahati nasibu kurudishwa