Mkuu wa Wilaya ya Magu mkoani Mwanza Salum Kali amekanusha habari iliyoandikwa na baadhi ya vyombo vya habari kuibwa kwa baadhi ya viungo vya miili ya marehemu kwenye makaburi yaliyovunjwa katika Wilaya ya Magu mkoani Mwanza.

Akizungumza na Dar24Media DC Salum amesema kuwa vijana wanaosadikiwa kuwa ni wavutaji wa madawa ya kulevya na walevi wamevunja misalaba iliyosimikwa na zege katika makaburi hayona kuipeleka misalaba hiyo kuiuza kama vyuma chakavu.

Aidha amesema kuwa kaburi moja ndio kaburi ambalo wamelivunja lakini pia wamechukua misalaba katika makaburi mengine, huku akisema kuwa hajathibitisha kuchukuliwa kwa viungo vya marehemu.

“Sijathibitisha na sitaki kuthibitisha ninachojua wamebomoa makaburi nimeyaona mwenyewe na bahati mbaya sana wamechukua vyuma chakavu na kuna maeneo wameharibu malumalu walizojengea lakini sio kwamba malumalu wamezichukua,” Amesema DC Salum.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Wilaya hiyo amesema kuwa, hadi sasa watu watatu wanashikiliwa kwa tuhuma za kubomoa makaburi hayo na kuiba misalaba na kwamba uchunguzi utakapokamilika watafikishwa mahakamani.

MEWATA wamshukuru Rais Samia
TBS yatoa leseni 303 kwa wajasiriamali