Vikosi vya usalama vya Iran vimewaua kwa kuwapiga risasi waandamanaji watatu, katika maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka mitatu ya umwagaji damu huku wafanyakazi wakigoma na wanafunzi wa vyuo vikuu wakisusia masomo katika wilaya ya Kurdistan, anakotokea Amini Mahsa, magharibi mwa Iran.
Wanaharakati vijana, wamewahimiza watu kujitoa ili kuiteka miji ya Ahvaz, Isfahan, Mashhad na Tabriz na mji mkuu Tehran, ambapo Maduka yalifungwa katika soko maarufu la biashara la Bazaar na viunga vyake, huku yakichochewa pia na kifo cha binti Mahsa Amini (22), aliyefariki mikononi mwa Polisi wa maadili, baada ya kukamatwa kwa madai ya kukiuka kanuni za mavazi ya wanawake nchini Iran.
Waandamanaji walimiminika barabarani baada ya kuitikia wito wa kuwakumbuka waliouawa katika ghasia za mwaka 2019, na kuongeza petroli kwenye moto kwa maandamano ya hivi karibuni yaliyochochewa na kifo cha Mahsa Amini, binti mwenye umri wa miaka 22, aliyefariki mikononi mwa polisi wa maadili baada ya kukamatwa kwa madai ya kukiuka kanuni za mavazi ya wanawake nchini Iran.
Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa, imeitaka Iran kuwaachilia mara moja maelfu ya watu waliokamatwa kwa kushiriki maandamano na kupitia msemaji wake, Jeremy Laurence amewambia waandishi wa habari mjini Geneva kuwa, “Kufikia tarehe 12, vikosi vya usalama vimetumia nguvu kupita kiasi na kusababisha mauaji ya watu wasiopungua 326, wakiwemo watoto 43 na wanawake 25.”