Wakazi wa Kijiji cha Madobole Kata ya Luponde Wilayani Njombe pamoja na Shirika la Watawa wa Kanisa Katoliki wa Jimbo la Njombe wametakiwa kutumia busara kumaliza mgogoro wa ardhi uliodumu kwa zaidi ya miaka 13.
Wito huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Christopher Ole Sendeka mara baada ya kutembelea eneo lenye mgogoro na kusikiliza pande hizo mbili zinazogombea eneo lililopo ndani ya eneo linalodaiwa kumilikiwa kisheria na Watawa hao.
“Tutawatuma wataalamu hapa wachukue ramani ya shamba hilo lote namba 535 waje wapitie mipaka vizuri na waniambie watu wako sehemu gani, halafu tuje tukae tuone tunatokaje, nia yangu nikuona ni lazima tunamaliza mgogoro huu kwa misingi ya kufuata sheria lakini pia kwa kujenga mahusiano kati ya waliopewa eneo, na wananchi waliokuwa wanajipatia ridhiki katika eneo hili ili kila mmoja awe huru kufanya shughuli zake,”amesema Ole Sendeka
Aidha, mara baada ya kumaliza kukagua eneo hilo, Ole Sendeka amezungumza na wananchi, Viongozi wa Siasa pamoja na Watawa ili kusikiliza malalamiko yao ambapo bado kumeonekana na shida katika kumaliza mgogoro huo.
-
Wananchi Ludewa wachimba Barabara kwa mikono
-
Mahakama yapiga chini shauri la kupinga Muswada wa Vyama vya Siasa
-
Kesi ya ‘Uchochezi’ inayomkabili Zitto Kabwe yaota Mbawa
Hata hivyo, kutokana na hali hiyo Mkuu wa Mkoa wa Njombe alitoa uamuzi wa kuitisha kikao cha pamoja ofisini kwake kati ya pande hizo zilizopo kwenye mgogoro ili kujadili kwa kina na kumaliza mgogoro huo.