Kufuatia ukiukwaji wa sheria ya ununuzi wa vifaa tiba vyenye thamani ya shilingi 3.4 billion kutoka kampuni ya Misri ya Al Andasia, jumla ya Watendaji saba wa Bohari ya Dawa Nchini – MSD, wameondolewa kazini.

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu ameyasema hayo Bungeni Jijini Dodoma wakati akijibu hoja zilizoibuliwa na Kamati za PAC, PIC na LAAC katika ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali – CAG, ya mwaka 2021/2022.

Amesema, “Serikali imechukua hatua za kiutawala ambapo ilimuondoa Mtendaji Mkuu wa Bohari ya Dawa mwezi Aprili 2022 pamoja na Wakurugenzi wengine sita akiwemo wa Utawala, Fedha na mipango, Ununuzi, Usambazaji wa huduma za kanda, Meneja wa Sheria na Mkaguzi Mkuu wa ndani wa MSD.”

Aidha Ummy amesema pia ulifanyika ukaguzi maalum wa eneo la ununuzi na kubadilisha watumishi 24 kabla ya CAG kati ya Juni – Desemba 2022, huku akidai utendaji wa sasa wa Bohari ya Dawa umeimarika baada ya kuongeza thamani ya bidhaa zilizosambazwa kutoka Bilioni 315 mwaka 2021/2022 hadi kufikia Shilingi Bilioni 373 mwaka 2022/2023.

EWURA yatoa onyo uuzaji holela wa Mafuta
Vijana watakiwa kuzitambua fursa za kiuchumi