Mkuu wa Wilaya ya Njombe, Ruth Msafiri amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Njombe Kuhakikisha anawahamisha bila malipo yeyote kama adhabu maofisa Watendaji watakaobainika kujihusisha na utoroshaji mapato ya Halmashauri ili kudhibiti mianya ya Utoroshaji mapato hayo.

Ametoa agizo hilo katika kikao cha Baraza la Madiwani Halmashauri ya wilaya hiyo kufuatia kuwepo kwa ujanja ujanja unaofanywa na baadhi ya maofisa ambao wanajihusisha na utoroshaji mapato na kuisababishia Serikali kupata hasara.

Halmashauri ya wilaya ya Njombe katika kipindi cha mwaka wa fedha 2018/2019 Imefikia asilimia 82 ya ukusanyaji mapato yake ya ndani hatua ambayo inaelezwa kuwepo kwa uwezekano mkubwa wa kufikia asilimia 100 ya ukusanyaji mapato ifikapo Juni 30 mwaka Huu.

Aidha, Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya hiyo, Valentino Hongoli amesema kuwa asilimia za ukusanyaji mapato zinatakiwa kuongezeka ili kufikia malengo kabla ya kuanza mwaka mpya wa fedha mwezi Julai 2019 na kuongeza kuwa licha ya kufikia asilimia 82 ya ukusanyaji mapato bado wanajipanga kuhakikisha Halmashauri yake inatekeleza agizo hilo la mkuu wa wilaya ya Njombe.

Pia ameongeza kuwa Utendaji kazi mzuri wa wataalamu katika Halmashauri ya wilaya ya Njombe umeifanya Halmashauri hiyo kupata hati safi kwa mwaka wa fedha 2017/2018 ikiwa baadhi ya madiwani akiwemo Diwani wa kata ya Igongolo, Isaya Japhet Myamba na Daina Mangula ambaye ni Diwani wa Viti Maalumu kukiri uwepo wa usimamizi mzuri katika ukusanyaji mapato.

Kwa upande wa mapato ya ndani katika mwaka wa fedha 2018/2019 Halmashauri ya wilaya ya hiyo ilipanga kukusanya pesa za kitanzanioa jumla ya bilioni 1.4, hadi kufikia mwezi machi mwaka huu wamekusanya kiasi cha Shilingi bilioni 1.1 sawa na asilimia 82 ya lengo la kukusanya bilioni 1.4.

Sababu yatajwa wanaume wengi kukosa nguvu za kiume
Hii ni ajabu kweli, unafungwa uko nyumbani?- JPM