Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali, Marco E. Gaguti amegawa vitambulisho 35,000 vya awamu ya pili vya Wafanyabiashara Wadogo wadogo katika Mkoa wa Kagera na kuwaagiza Watendaji wa Serikali chini ya usimamizi wa Wakuu wa Wilaya kuendelea na zoezi la ugawaji wa vitambulisho hivyo na kuhakikisha ifikapo Februari 28, 2019 vitambulisho vyote viwe vimegawiwa kwa Wafanyabiashara Wadogo.
 
Amesema kuwa katika tathimini iliyowakutanisha Wakuu wa Mikoa 26 ya Tanzania Bara Mkoa wa Kagera haukufanya vizuri sana wala vibaya katika ugawaji wa vitambulisho vya awamu ya kwanza 25,000 kwani ulishika nafasi ya sita kwa ugawaji wa asilimia 65%.
 
Ameziagiza Mamlaka za Serikali za Mitaa kuhakikisha zinakusanya takwimu za Wafanyabiashara wote Wakubwa, wa Kati na wale Wadogo ifikapo Februari 15, 2019 takwimu hizo ziwe zimewasilishwa ofisini kwake lengo likiwa ni kuhakikisha kila mwananchi anayetoa bidhaa yoyote na kupokea fedha anatambuliwa na kulipa kodi au tozo stahiki za Serikali.
 
Aidha, hafla hiyo fupi iliyowashirikisha Wakuu wa Wilaya saba za Mkoa wa Kagera, Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri za Wilaya na Manispaa, Wenyeviti wa Halmashauri na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Bukoba, Watendaji wa Kata wa Manispaa ya Bukoba waliowawakilisha Watendaji wenzao katika mkoa ambao walitakiwa kutoa changamoto zinazowakumba katika ugawaji wa vitambulisho vyaWafanyabiashara Wadogo wadogo katika maeneno yao.
  • Sakata la CAG, Spika Ndugai Mahakama yatoa uamuzi
 
  • Serikali kuongeza nguvu sekta binafsi
 
  • Kikosi Maalum cha Polisi chatua mkoani Njombe
Wakitoa changamoto mbalimbali kuhusu ugawaji wa vitambulisho Watendaji wa Kata wamesema kuwa changamoto kubwa ni Elimu kwa wananchi kutojua ni mfanyabiashara yupi anatakiwa kupata kitambulisho na ni yupi hastahili kupata na changamoto hiyo inatokana na suala la mauzo ghafi kutoeleweka vizuri kwao Watendaji kama wahusuika wa ugawaji lakini pia wafanyabiashara jambo ambalo waliitaka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kutoa uelewa kwao.
 
Changamoto nyingine iliyotajwa na Watendaji ni suala la Mfanyabiashara Mdogo kuwa na namba ya utambuzi ya mlipa kodi ya TRA (TIN) wakati biashara yake ni ndogo na hastahili kupata kitambulisho cha mfanyabiashara mdogo wakati mtaji wake ni mdogo haufikii kiwango cha shilingi milioni 4,000,000/= kwa mwaka.
 
Hata hivyo, Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Mkoa wa Kagera, Adam Ntoga amesema kuwa Mfanyabiashara Mdogo anayestahili kupata kitambulisho ni yule ambaye mauzo yake kwa siku hayafikii shilingi 11,000/= kwa siku. Kama Mfanyabiashara anauza bidhaa zake na kupata kiwango cha fedha chini ya shilingi 11,000/= huyo anastahili kupata kitambulisho cha Mfanyabiashara Mdogo.

Video: Bunge laibua ubadhirifu wa Sh31 bilioni za umma, Miradi saba bomu NSSF
Bajeti ya Shil. Bil. 50.4 kutekeleza miradi ya maendeleo Bukoba 2019/2020