Rais Dkt. John Pombe Magufuli leo Julai 17, 2020 amemteua Dkt. Jumanne Fhika aliyekua Ofisi ya Rais kuwa Mkuu mpya wa Mkoa wa Njombe akichukua nafasi ya Christopher Ole Sendeka.

Mheshimiwa Rais pia amebadili kituo cha kazi kwa Josephat Paulo Maganga aliyekua Mkuu wa Wilaya ya Geita kuwa Mkuu wa Wilaya ya Dodoma akichukua nafasi ya Patrobas Katambi huku.

Na aliyekua Mwenyekiti wa CCM Lindi Fadhili Mohamed Juma akiteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Geita.

Aidha, Rais John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Aloyce Nzuki kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii. Kabla ya uteuzi huo, Dkt. Nzuki alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii na anachukua nafasi ya Profesa Adolf Mkenda.

Rais Magufuli amemteua aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Dkt. Seif Shekilage kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Songwe, akichukua nafasi ya David Kafulila. Nafasi ya Shekilage ya Ukuu wa Wilaya Maswa inachukuliwa na Aswege Enock.

Wakati huohuo Rais Magufuli amemteua Mussa Chogelo kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala, akichukua nafasi ya Sophia Mjema. Kabla ya uteuzi Chogelo alikuwa Ofisi ya Rais.

Rais Magufuli amemteua pia Dkt.Athman Kihamia kuwa DC Rombo akichukua nafasi ya Agness Hokororo na amemteua pia Calorious Misungwi kuwa DC Kalambo akichukua nafasi ya Julieth Binyura, Wateule wote.

Mkuu wa nchi pia amemteua Mhandisi Anthony Sanga kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji ambapo kabla ya uteuzi huo, Mhandisi Sanga alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na anachukua nafasi ya Prof. Kitila Alexander Mkumbo.

Wengine walioteuliwa ni Dr. Allan Kijazi kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii akichukua nafasi ya Dkt. Aloyce Nzuki, pia Dr. Kijazi ataendelea kuwa Kamishna wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA).

Mhandisi Nadhifa Kemikimba ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji ambapo kabla ya uteuzi huo alikuwa Mkurugenzi katika Wizara ya Maji na anachukua nafasi ya Mhandisi Anthony Sanga ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji.

Askari 'ambaka' mgonjwa wa corona aliyekuwa anamlinda
Waziri Mkuu ahimiza viongozi wa dini kulinda amani