Mkurugenzi wa tiba Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na watoto Dkt Grace Magembe amewahasa watoa huduma za afya nchini kufanya kazi kwa juhudi kwa kuzingatia maadili wakati wa kumuhudumia mgojnwa.

Ameyasema hayo wakati wa ziara ya ukaguzi wa hali ya utoaji huduma ya afya na ujenzi wa miundombinu katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara.

“Serikali imewekeza kwenye miundombinu, kwenye vifaa tiba, hali ya upatikanaji wa dawa lakini watumishi wanatakiwa wafanye kazi kwa weledi kwa kuzingatia maadili ya kazi zao wakati wa kumuhudumia mgojnwa” Amesema Dkt Grace.

Aidha Dkt Grace amesema kwa kiasi kikubwa ameridhishwa na hali ya upatikanaji wa dawa katika maeneo aliyofanyia ziara, huku akitoa rai kwa watoa huduma kuhakikisha mngojnwa anapoandikiwa dawa azipate dawa alizoandikiwa kwa muda sahihi.

Sambamba na hilo Dkt Grace amewakumbusha agizo la Mganga Mkuu wa serikali Prof. Abel Makubi juu ya kufanya kazi kwa juhudi na ushirikiano ili kupunguza vifo vya mama na mtoto, na kuweka mikakati thabiti katika mapambo dhidi ya vita hiyo.


Babu wa Kenya akaribia kutua Msimbazi
Young Africans kushtaki TFF